Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga Mbongo atambulishwa Ujerumani

WINGA Pict

Muktasari:

  • Mwanadada huyo anakuwa Mtanzania wa kwanza kuitumikia ligi ya Ujerumani kwa upande wa wanawake.

WINGA wa Kitanzania, Emma Lattus ametambulishwa kwenye kikosi cha timu ya Borussia Monchengladbach inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Ujerumani akitokea FC Koln 2.

Mwanadada huyo anakuwa Mtanzania wa kwanza kuitumikia ligi ya Ujerumani kwa upande wa wanawake.

Licha ya nyota huyo (18) mwenye asili ya nchi mbili, Tanzania na Ujerumani, klabu hiyo inamtambua kama Mtanzania.

"Borussia imemsajili Emma Lattus kutoka 1. FC Cologne. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 mwenye asili ya Kitanzania anakuja kucheza katika nafasi ya wingi, Sogeza pembeni usome maneno ya kwanza kutoka kwa usajili wetu wa kwanza mpya," ujumbe wa Instagram ulimtambulisha nyota huyo.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Emma alisema ilikuwa ndoto yake kubwa kusajiliwa na timu hiyo yenye malengo makubwa ya kucheza Ligi Kuu.

"Ninafuraha sana kusajiliwa na Borussia, ilikuwa ndoto yangu ya siku nyingi kuichezea timu hii yenye malengo ya kucheza Ligi Kuu," alisema Emma.

Winga huyo alizaliwa jijini Dar es Salaam, mama yake ni Mtanzania na baba yake ni raia wa Ujerumani.

Wazazi wake hawakukaa muda mrefu Tanzania kwani baadaye walihamia moja kwa moja Ujerumani ambako hadi sasa wanaishi na familia yake.