Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haji Mnoga asaini mwaka mmoja England

MNOGA Pict

Muktasari:

  • Mnoga alisajiliwa na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja uliokuwa unaisha mwishoni mwa msimu huu.

BEKI wa Salford City na timu ya Taifa, Taifa Stars, Haji Mnoga ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia katika kikosi hicho kinachoshiriki League Two (daraja la nne) nchini England.

Mnoga alisajiliwa na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja uliokuwa unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Mmoja wa watu wa karibu wa mchezaji huyo, aliliambia Mwanaspoti kuwa, juzi beki huyo wa kulia alisaini mkataba wa mwaka mmoja.

Aliongeza, isingekuwa rahisi kwa klabu hiyo kumuachia Mnoga kutokana na umuhimu wake kikosini hapo.

"Tunashukuru jambo limekwenda vizuri na ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja alisaini Jumatatu jioni baada ya kuelewana," amesema mtu huyo.

Huu utakuwa msimu wa pili kwa Mtanzania huyo kukipiga Salford ya England akitokea Aldershot aliyeichezea kwa misimu miwili.
Mnoga alicheza mechi 39 kati ya 46 zilizocheza timu hiyo kwa dakika 3,306 ambazo amekuwa mhimili mkubwa kwenye kikosi hicho.

Tangu asajiliwe kikosini hapo amekuwa beki wa pembeni tegemeo na kuwaweka benchi nyota mbalimbali kwenye eneo hilo akifunga bao moja na kutoa asisti nne.

Ligi ya nchi hiyo imetamatika na Salford inayomilikiwa na nyota wa zamani wa Manchester United, David Beckham na Garry Naville imemaliza katika nafasi ya nane katika mechi 46 imeshinda 18, sare 15 na kupoteza 13 ikikusanya pointi 69.