Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubingwa WPL... Yanga yatibua hesabu za Simba

Muktasari:

  • Yanga Princess ilikubali kichapo hicho kwenye Uwanja wa KMC Complezxx, Mwenge Dar es Salaam na kuiwezesha JKT kurejea kileleni ikiing'opa Simba Queens inayotetea taji hilo ililotwaa msimu uliopita ikiwa ni mara ya nne kwao na kuwa vinara wa kubeba mara nyingi ubingwa wa Ligi hiyo.

KIPIGO cha mabao 2-0 ilichopata jioni hii Yanga Princess mbele ya JKT Queens kimetibua hesabu za watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), Simba Queens katika mbio za ubingwa kwa msimu huu.

Yanga Princess ilikubali kichapo hicho kwenye Uwanja wa KMC Complezxx, Mwenge Dar es Salaam na kuiwezesha JKT kurejea kileleni ikiing'opa Simba Queens inayotetea taji hilo ililotwaa msimu uliopita ikiwa ni mara ya nne kwao na kuwa vinara wa kubeba mara nyingi ubingwa wa Ligi hiyo.

Bao la mapema la dakika ya tano lililofungwa na Jamila Rajabu aliyemalizia pasi ya Stumai Abdallah na lile la pili kupitia kwa kinda Winifrida Gerald katika dakika ya 14 yaliizima Yanga na kuwarejesha maafande hao kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Simba.

Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa msimu huu katika Ligi hiyo kwa JKT dhidi ya Yanga, kwani mechi ya duru la kwanza ilishinda pia 2-0 mabao yote yakifungwa na Donisia Minja.

Mechi ya jioni ya leo ilikuwa ni ta raundi ya 16 kwa WPL, baada ya juzi Simba iliyoka sare ya 2-2 na mabinti wa Mapigo na Mwendo, Mashujaa Queens na kuifanya ifikishe pointi 41 kabla ya JKT kuzifikia, lakini ikibebwa na mabao ya kufunga na kufungwa, huku kila moja ikisaliwa na mechi mbili mkononi kufunga msimu.

JKT imevuna jumla ya mabao 61, huku ikifungwa saba tu, ilihali Simba imefunga mabao 52 na kufungwa 13, kitu kinachofanya mbio za ubingwa kusubiriwa kuona kama itaamuliwa kwa tofauti hayo ya mabao au kuna maajabu yatakayotokea baina ya timu hizo mbili.

Kipigo cha leo kimeifanya Yanga Princess kuendelea kusalia nafasi ya tatu ikiwa imekusanya  pointi 33 baada ya kucheza mechi 16, ikiwa imesaliwa pia na mechi mbili kufungia msimu.

Simba ina mechi dhidi ya Bunda Queens na Alliance Girls. ilihali JKT yenyewe itakutana na Fountain Gate Princess na Gets Progam inayocheza ligi hiyo kwa mara ya kwanza na inashika nafasi ya tisa kati ya timu 10 katika msimamo wa lLigi hiyo iliyoasisiwa msimu wa 2015-2016, ambapo Mlandizi Queens iliyorejea tena msimu huu na kushuka mapema, ndio iliyokuwa mabingwa wa kwanza.

Timu nyingine zilizotwaa ubingwa huo ni JKT Queens iliyotwaa mara tatu, ikiwamo mbili mfululuizo ilipoipokea Mlandizi 2016-2017 na 2017-2018 kisha kurudia tena miwili miwili iliyopita, wakati Simba ndio kinara ikitwaa mara nne ikiwamo taji la msimu uliopita ambalo inaliletetea kwa sasa.