Tanzania kuanza na Sudan Cecafa Dar MASHINDANO ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ya Wanawake yanatarajiwa kuanza Juni 12, mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex ambapo Tanzania itaumana na Sudan Kusini.
Lunyamila kumaliza ukame wa mabao FC Juarez USAJILI wa nyota mpya Mtanzania, Enekia Lunyamila aliyetua FC Juarez huenda ukamaliza tatizo la ufungaji mabao katika klabu hiyo kutokana na rekodi zake nzuri alikotoka.
Chomelo: Haukuwa msimu mzuri, tutajipanga KIUNGO wa Konya Amputee inayoshiriki Ligi ya Walemavu Uturuki, Ramadhan Chomelo amesema haukuwa msimu mzuri kwa upande wao kutokana na ushindani kuongezeka huku kwa upande wake akitakiwa kufanya...
Miroshi ashindwa kuandika rekodi Ulaya KIRAKA wa Goztepe inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki, Novatus Dismas Miroshi ameshindwa kuandika historia nyingine kwenye michuano ya Ulaya baada ya chama lake kumaliza nafasi ya nane kwenye...
Majeraha yamtibulia Kachwele Marekani STRAIKA wa Whitecaps FC anayecheza kwa mkopo Vancouver Whitecaps inayoshiriki Ligi Kuu Marekani (MLS), Cyprian Kachwele amesema msimu huu ameuanza vibaya baada ya kupata majeraha ya nyama za paja.
JKT Queens yaanza na kocha WAKATI JKT Queens ikijiandaa na mashindano ya Cecafa ili kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika imeanza marekebisho ya benchi la ufundi ikidaiwa kumalizana na kocha mkuu Ester Chabruma ‘Lunyamila’.
Hili hapa Chama la Baum Ujerumani WIKI zilizopita RB Leipzing ilimtambulisha kiungo Lisa Baum ambaye ana asili ya nchi mbili Tanzania na Ujerumani.
Clara awavuruga mabosi Al Nassr MOTO wa mshambuliaji wa Kitanzania, Clara Luvanga unazidi kuwachanganya viongozi wa Al Nassr ya Saudia na inaelezwa wako kwenye mchakato wa kumboreshea mkataba wake uliosalia mwaka mmoja.
Beki KMC mambo bado Al Hilal BEKI wa pembeni wa KMC, Raheem Shomary aliyeripotiwa kupewa ruksa ya kwenda kujiunga na Al Hilal ya Sudan, amekiri mambo bado, kwani hakijaeleweka, ila anajipa moyo muda si mrefu kila kitu...
Mwalimu anaingia katika mfumo KITENDO cha mshambuliaji wa Kitanzania, Seleman Mwalimu ‘Gomez’ kucheza dakika 10 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya Wydad AC na Sevilla, kimewaibua makocha wakimsifu kuwa anaingia...