Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Clara awavuruga mabosi Al Nassr

CLARA Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa nyota huyo mwenye makombe mawili ya Ligi Kuu ya Wanawake Saudia yuko nchini kwenye majukumu ya timu ya taifa, Twiga Stars ambayo iko Dar es Salaam kucheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki kujipima nguvu kabla ya kwenda WAFCON.

MOTO wa mshambuliaji wa Kitanzania, Clara Luvanga unazidi kuwachanganya viongozi wa Al Nassr ya Saudia na inaelezwa wako kwenye mchakato wa kumboreshea mkataba wake uliosalia mwaka mmoja.

Kwa sasa nyota huyo mwenye makombe mawili ya Ligi Kuu ya Wanawake Saudia yuko nchini kwenye majukumu ya timu ya taifa, Twiga Stars ambayo iko Dar es Salaam kucheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki kujipima nguvu kabla ya kwenda WAFCON.

Katika mechi ya kwanza dhidi ya Congo, Clara alifunga bao moja na kufanya Tanzania iibuke na ushindi wa 2-1, katika mchezo ambao mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga Princess alionyesha kiwango bora.

Chanzo cha kuaminika kililiambia Mwanaspoti kuwa mabingwa hao wanamuandalia ofa ya maana nyota huyo tishio kwenye ligi ya Saudia.

Hata hivyo, kiliongeza kuwa tayari kuna ofa kadhaa zimeanza kuletwa na timu mbalimbali duniani kumuhitaji Luvanga aliyemaliza na mabao 21 msimu huu.

“Al Nassr bado inamuhitaji sasa kuna ujanja wa kupiga pesa wanataka kuufanya kwa sababu kuna baadhi ya klabu duniani hasa Marekani zimeanza kumfuatilia,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Wanachotaka kufanya ni kumboreshea mkataba ili ofa watakayoiweka Nassr kwa timu zinazomuhitaji Clara ziendane na thamani yake na hivyo kiasi kikubwa kitarudi kwa timu.”

Ikumbukwe Clara anasimamiwa na kampuni ya LTA Agency inayosimamia wachezaji mbalimbali duniani akiwamo Mzambia Barbra Banda anayekipiga Orlando Pride ya Marekani, Aisha Masaka wa Brighton ya England na Irene Paredes anayekipiga Barcelona ya Wanawake.