Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dalali abaini jambo Simba, Yanga

DALALI Pict

Muktasari:

  • Simba imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu ikipoteza mbele ya RS Berkane ya Morocco, ikiwa ni misimu miwili tu tangu Yanga ilipotinga na kupoteza taji kwa kanuni ya bao la ugenini dhidi ya USM Alger ya Algeria baada ya matokeo jumla kuwa sare ya 2-2.

MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ‘Field Marshal’ amesema amezifuatilia kwa karibu Simba na Yanga katika michuano ya kimataifa ya CAF na kushtukia jambo ambalo kama klabu hizo zitarekebisha kidogo tu, basi muda si mrefu zitabeba ubingwa wa Afrika.

Simba imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu ikipoteza mbele ya RS Berkane ya Morocco, ikiwa ni misimu miwili tu tangu Yanga ilipotinga na kupoteza taji kwa kanuni ya bao la ugenini dhidi ya USM Alger ya Algeria baada ya matokeo jumla kuwa sare ya 2-2.

Dalali alisema klabu hizo kongwe nchini zipo katika nafasi nzuri ya kuleta taji la Afrika, ila ni lazima zirekebishe vitu anavyoamini vimezinyima ubingwa kwa misimu miwili tofauti iliyopita.

Dalali aliyeiongoza Simba kati ya mwaka 2007-2010, alisema ni wakati wa timu hizo kuwekeza katika usajili utakaoendana na michuano ya CAF, kwa kushusha mashine za maana zitakazoweza kumudu mikiki ya kukabiliana na wapinzani wao na hapo ndipo itaandikwa historia mpya nchini.

“Kiufundi Simba na Yanga kwa ukubwa wao zinahitaji kusajili wachezaji wenye uwezo utakaoendana na michuano ya CAF, wakifanya hilo naamini taji la CAF lipo wazi, ingawa wakati mwingine changamoto zinakuwa kwa waamuzi, lakini ukiwa vizuri uwanjani ni rahisi kufanya maajabu,” alisema Mzee Dalali aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Matawi ya Mkoa wa Dar es Salaam aliyeongeza;

“Sina maana wachezaji waliopo ni wabaya, ila wanahitaji kuongezewa nguvu, mfano Simba katika usajili wa msimu huu nashauri waongezee mabeki wa pembeni wa kuwasaidia Shomari Kapombe na Mohemed Hussein ‘Tshabalala’, mshambuliaji na beki wa kati.”

Alikiri licha ya Simba kufanya kazi kubwa hadi kutinga fainali ya CAF kiuwezo RS Berkane ilikuwa na wachezaji ghali na viwango vikubwa, jambo lililomfanya asisitize ni wakati wa klabu kongwe kuonyesha ukubwa wao Afrika.

Mbali na kuzitaka Simba na Yanga zijipange katika usajili, alizungumzia dabi kwamba kipindi ambacho aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanajangwani marehemu Imani Madega timu hiyo iliwahi kutotokea uwanjani.

“Ingawa matukio yalikuwa tofauti ila nilipompigia simu Madega kumuuliza wako wapi alisema wamejikuta wako Kimbiji, kuhusu dabi ya Juni 15 nitakwenda uwanjani kuisapoti timu kama Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ilivyoelekeza,” alisema.

Katika uongozi wake aliacha alama mbalimbali kama kuanzisha Simba Day mwaka 2009 inayofanyika hadi sasa mbali na kuweka rekodi ya Simba kubeba ubingwa bila kupoteza msimu wa 2009-2010 kabla ya kuja kuvunjwa na Azam FC msimu wa 2013-2014 na Yanga kuiboresha zaidi 2021-2021.