Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu anaingia katika mfumo

MWALIMU Pict

Muktasari:

  • Wydad imecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Sevilla na Porto kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia inayotarajiwa kuanza Juni 15, 2025 hadi Julai 13, 2025 nchini Marekani.

KITENDO cha mshambuliaji wa Kitanzania, Seleman Mwalimu ‘Gomez’ kucheza dakika 10 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya Wydad AC na Sevilla, kimewaibua makocha wakimsifu kuwa anaingia kwenye mfumo wa timu hiyo taratibu.

Wydad imecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Sevilla na Porto kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia inayotarajiwa kuanza Juni 15, 2025 hadi Julai 13, 2025 nchini Marekani.

Mechi ya kwanza dhidi ya Sevilla, Mwalimu aliingia katika dk80, na alionyesha ukomavu mkubwa, kasi na maarifa ya kutoa pasi kwa walengwa.

Kocha wa Alliance, Sultan Juma alisema pamoja na ugumu wa ligi hiyo, bado anaiona nafasi ya nyota huyo kuanza mbele ndani ya kikosi cha Wydad.

“Unajua sasa hivi amebadilika sana, kuanzia anapopokea mali anaendana na kasi ya soka lao la ushindani, mechi ya juzi alikuwa mtulivu sana sema kuna muda alizidiwa uzoefu na Sevilla,” alisema Juma.

Kocha wa Ceasiaa, Ezekiel Chobanka alisema nyota huyo ameanza kukua na kuingia kwenye mfumo wa timu hiyo na anaona akifanya makubwa siku zijazo kama ataendelea kupewa nafasi.

“Umri wake bado mdogo ana vitu vingi vya kufanya kwenye mpira lakini kwa hivi karibuni amebadilika sana tuliokuwa tunafatilia Ligi Kuu Bara na sasa kuna utofauti.”

Gomez alijiunga na Wydad Januari 31, 2025 akitokea Singida Black Stars kwa mkataba wa hadi Juni 30, 2029 na anaungana na Aziz KI aliyetambulishwa hivi karibuni akitokea Yanga alipodumu ndani ya misimu mitatu.

Wydad ni kati ya timu 32 zitakazoshiriki michuano hiyo huku wawakilishi wengine wa Afrika ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Esperance (Tunisia) na Al Ahly (Misri).

Katika michuano hiyo, Wydad imepangwa Kundi G na timu za Manchester City ya England, Al Ain (United Arab Emirates) na Juventus (Italia).

Mechi ya kwanza Wydad itacheza Juni 18 dhidi ya Manchester City, kisha Juni 22 dhidi ya Juventus na kumaliza hatua ya makundi Juni 26 ikipambana na Al Ain.