Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania kuanza na Sudan Cecafa Dar

CECAFA Pict

Muktasari:

  • Timu tano kutoka ukanda wa Cecafa zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo yatakayomalizika Junie 21 yakijumuisha Burundi, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania na bingwa mtetezi, Uganda.

MASHINDANO ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ya Wanawake yanatarajiwa kuanza Juni 12, mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex ambapo Tanzania itaumana na Sudan Kusini.

Timu tano kutoka ukanda wa Cecafa zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo yatakayomalizika Junie 21 yakijumuisha Burundi, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania na bingwa mtetezi, Uganda.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Cecafa, Yusuf Mossi ameeleza kuwa Tanzania, Uganda, Burundi na Sudan Kusini zimethibitisha kushiriki hadi sasa.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yamepangwa kufanyika kabla ya yale Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (Wafcon) yatakayofanyika mwezi ujao.

"Mashindano haya yatawasaidia wawakilishi wetu, Tanzania, kujiandaa vyema kwa Wafcon, na pia yataziwezesha timu nyingine kujiandaa kwa mechi za kufuzu Wafcon 2026 zitakazoendelea Oktoba mwaka huu," amesema Mossi.

Ikumbukwe Zanzibar ilikuwa timu ya kwanza kuandika historia kwenye mashindano hayo yaliyoanzishwa 1986 kwa kuchukua ubingwa.

Hata hivyo, mashindano hayo hayakuendelea kwa takriban miaka 30 ingawa kulikuwa na jitihada za kuyarudisha na 2007 yalifufuliwa yakipigwa Zanzibar na baadaye yakafutwa na hayakuchezwa tena.

Mwaka 2016 yalirejeshwa tena na Uganda ikawa mwenyeji, na Tanzania iliibuka bingwa wa mashindano hayo, huku 2018 Tanzania ikitetea ubingwa ikitwaa kwa mara ya pili mfululizo.

Ubingwa wa mara mbili mfululizo uliifanya Tanzania 2019 kupewa heshima ya kuwa mwenyeji. Hata hivyo, ilishindwa kutetea mara ya tatu baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Kenya.

Mwaka 2021 hayakuchezwa kutokana na marekebisho ya uwanja yaliyokuwa yakiendelea nchini Djibouti ambako yalipangwa kufanyika na msimu uliofuata Uganda ikanyakua taji hilo baada ya kuichapa Burundi mabao 3-1 kwenye fainali iliyopigwa mjini Jinja, Uganda.