Lwanga, Onyango, Bwalya warejea Simba

KIKOSI cha Simba kimeendelea kuimarika baada ya nyota wake watatu Joash Onyango, Rally Bwallya na Taddeo Lwanga waliokuwa wakizitumikia timu zao za taifa kurejea.

Lwanga alikuwa katika timu ya taifa ya Uganda, Onyango Kenya na Bwalya Zambia ambao wote walikuwa wakizitumikia timu hizo za mataifa yao katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Mwananchi Digital leo jioni limewashuhudia watatu hao wakirejea mazoezini katika Uwanja wa Boko Beach Veteran ambapo waliwasili na basi kubwa la wachezaji wakiambatana na wachezaji wengine wa kikosi hicho.

Baada ya kuwasili kila mchezaji alijiandaa tayari kwa mazoezi na kisha kuanza mazoezi na wenzao kama kawaida.

Wachezaji wengine Aishi Manula, John Bocco, Israel Mwenda, Mohamed Hussein, na Kibu Denis waliokuwa timu ya Taifa ya Tanzania wameendelea na mazoezi ya pamoja baada ya kurejea kambini jana.

Wachezaji wengine waliokuwa mazoezini leo ni Yusuph Mhilu,Benard Morrison, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, Pascal Wawa, Hannoc Inonga, Hassan Dilunga, Sadio Kanoute, Abdulsamad Kassim, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Ibrahim Ajibu,  Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jimmyson Mwanuke,Beno Kakolanya, Ally Salim, Jeremiah Kisubi na Ahmed Feruz.

Simba inajiandaa na mchezo wao kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana Oktoba 17 na timu hiyo inatarajia kusafiri Ijumaa Octoba 15 kuelekea Botswana kwenye mchezo huo.