Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki JKT mbioni kuibukia Msimbazi

Muktasari:

  • Beki huyo wa kati ni Wilson Nangu anayedaiwa menejimenti yake imeanza mazungumzo ya kusaini mkataba wa kujiunga na kikosi hicho ikichangiwa zaidi na kushindwa kumnasa beki wa Coastal Union, Lameck Lawi aliyekuwa akiwindwa tangu msimu uliopita na Simba ambaye alitua Azam  hivi karibuni.

SIKU moja tangu kuvuja kwa taarifa ya ripoti ya kocha wa Simba, Fadlu Davids kutaka asajiliwe majembe sita mapya ili kuunda kikosi bora cha msimu ujao akiwamo beki wa kati, Mwanaspoti limenasa jina la beki ambaye ameingia katika rada za Wekundu wa Msimbazi kutoka JKT Tanzania.

Beki huyo wa kati ni Wilson Nangu anayedaiwa menejimenti yake imeanza mazungumzo ya kusaini mkataba wa kujiunga na kikosi hicho ikichangiwa zaidi na kushindwa kumnasa beki wa Coastal Union, Lameck Lawi aliyekuwa akiwindwa tangu msimu uliopita na Simba ambaye alitua Azam  hivi karibuni.

Simba inafanya maboresho ya kikosi chake katika nafasi ya beki wa kati huku wachezaji wanaotajwa kuondoka ni mzawa Hussein Kazi aliyemaliza mkataba na wa kigeni, Che Fondoh Malone, hivyo inapambana kupata mbadala wao.

Chanzo cha habari kimesema: “Simba sio mara ya kwanza kuhitaji huduma ya Nangu. Iliwahi kufanya hivyo tangu akiwa TMA Stars ya Arusha inayoshiriki Ligi ya Championship. Ni kati ya majina ambayo yamependekezwa na kocha Fadlu Davids.

“Nangu bado ana mkataba na JKT Tanzania, viongozi (wa Simba) wanaangalia uwezekano wa kuuvunja na endapo makubaliano yakienda sawa lolote linaweza likatokea.”

Msimu uliomalizika Nangu alifunga mabao mawili na alikuwa katika kiwango bora ambacho kimeivutia Simba kuhitaji huduma yake ili akaongeze ushindani dhidi ya Abdulrazack Hamza.

“Kocha anahitaji ushindani kila nafasi anayeingia na kutoka wawe levo ileile ya kusaidia timu na siyo mmoja akiumia basi izuke wasiwasi kama ilivyowahi kutokea kwa Hamza alivyoumia mashindano ya kimataifa ikawa changamoto,” kilisema chanzo hicho.

Msimu uliomalizika Kazi alicheza dakika 10 pekee dhidi ya KMC na Che Malone alikuwa tegemeo kikosi cha kwanza akifunga mabao mawili.

Mbali na Hamza, Kazi na Che Malone, nyota mwingine anayecheza beki wa kati katika kikosi cha Simba ni Chamou Karaboue.