Ibenge rasmi Azam, afichwa hotelini

Muktasari:
- Kocha huyo mwenye mafanikio kwenye soka la Afrika, amewasili Dar es Salaam saa 11 jioni hii kumalizana na Azam FC na ataiongoza timu hiyo msimu ujao.
MWANASPOTI limejiridhisha kwamba Kocha maarufu raia wa DR Congo, Florent Ibenge yupo Dar es Salaam.
Kocha huyo mwenye mafanikio kwenye soka la Afrika, amewasili Dar es Salaam saa 11 jioni hii kumalizana na Azam FC na ataiongoza timu hiyo msimu ujao.
Mwanaspoti linajua kwamba Ibenge ambaye wakati fulani aliwahi kutakiwa na Simba na Yanga, amefikia kwenye hoteli moja maarufu iliyoko karibu na Mahakama ya Kisutu mita chache kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Azam imepania kufanya mabadiliko makubwa ndani na nje ya uwanja msimu ujao ili kufanya vizuri katika ligi ya ndani na michuano ya kimataifa.