Gomes amuanzisha Mkude, Simba ikiwakabili African Lyon

ZIKIWA zimesalia dakika chache kuanza kwa mchezo wa michuano Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Simba na African Lyon tayari vikosi vya timu zote mbili vitakavyocheza leo vimewekwa hadharani.

Simba ambao ni wageni katika mchezo huo wameonekana kufanya mabadiliko katika kikosi chao cha leo katika maeneo matatu kwa maana ya Beki, kiungo na Ushambuliaji.

Upande wa beki wa kulia ambao kwa mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly alipangwa Shomari Kapombe, leo hii ataanza Kennedy Juma huku koshoto alikozoeleka kucheza Mohammed Hussein ataanza Gadiel Michael.

Erasto Nyoni na Ibrahim Ame wanatarajiwa kucheza eneo la beki wa kati ambalo mchezo ulopita walicheza Paschal Wawa na Joash Onyango.

Katikati ya uwanja kwa maana ya kiungo, kocha mkuu wa timu hiyo Didier Gomes amemuanzisha Jonas Mkude ambaye kwa muda mrefu hajaonekana uwanjani kutokana na kusimamishwa kwa makosa ya kinidhamu ambayo hata hivyo yalitatuliwa.

Ibrahim Ajib pia ataanza leo sambamba na Rally Bwalya huku Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin walioanza kwenye mechi iliyopita dhidi ya Ahly wakipumzishwa.

Eneo la Ushambulia Meddie Kagere ndiye ataanza huku Parfect achikwende na Hassan Dilunga wakicheza kama mawinga.


VIKOSI KAMILI.

African Lyon: Bwanaheri Abdallah, Gody Sabasi, Paschal Kibandula, Mussa Januari, Emanuel Simwanza, Rehani Kibingu, Said Mtikila, Sadi Kipanga, Ramadhan Hashimu na Geofrey Mwashuiya.

Simba: Aishi Manula, Kennedy Juma, Gadiel Michael, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Rally Bwalya, Ibrahim Ajib, Meddie Kagere, Parfect Chikwende na Hassan Dilunga.