Wasanii wamiminika kumpongeza Samatta kutua Aston Villa

Tuesday January 21 2020

Wasanii wamiminika kumpongeza Samatta kutua Aston Villa-Wasanii na wanamichezo -mitandao ya kijamii -mshambuliaji nahodha wa Taifa Stars-Mbwana Samatta

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam.Wasanii na wanamichezo mbalimbali wamemiminika katika mitandao ya kijamii kutoa pongeza kwa mshambuliaji nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kwa kujiunga na Aston Villa kwa mkataba wa miaka minne na nusu.

Tangu kutoka kwa taarifa rasmi ya klabu Aston Villa kutangaza rasmi kumsajili Samatta akitokea KRC Genk ya Ubelgiji wasanii na watu mashuhuri nchini Tanzania kupitia mtandao wa kijamii Instagram wamempongeza Mbwana Samatta kwa kukamilisha tukio hilo tukufu.

Mwana FA "Kimsingi ni kuwa baada ya hii sina deni na EPL kwenye maisha yangu ya ushabiki wa mpira..asante Captain Diego @samagoal77 #HainaKufeli haswaaa..🙌🏽"

Ommy Dimpoz "Hongera Sana Captain Diego @samagoal77  @avfcofficial Umetupiga Gumi la Mgongo Acha tutembee kifua Mbele"

Haji Manara "chochote ntakachoandika hakitalingana na furaha niliyopata jana usiku.. Nenda Nenda Nenda Mwanamme.

Nna hakika kwa Dua hz utatoboa na hapo,,,kikubwa jua tupo watu sasa hv, Tutashabikia Aston Villa kama majuha!!! Samata The Pride of Nchi. 🙏🙏 @samagoal77"

Advertisement

Steve Nyerere "Niliwahi kusema miaka hiyo wakati nastafu kucheza Soka, Tunaitaji Mtu Atakayeweza kuwa Anajuhudi ya kufanikisha malengo yake katika soka, Uyu Kijana kachukua kila kitu nilichokuwa nafanya Enzi zangu kwenye Soka, Yani hajaniacha kabisa kila kitu changu nilichokuwa nafanya enzi zangu dooooo samata kachukua,,Kwakweli nakupongeza sanaa tena sanaa Mungu akupe Afya njema, Uko ndio Uangushe Mvua ya magoli balaaaaaaaaaa Najua hujawahi kukosea macho ya watanzania yote yapo kwako, Amna kufeli hahahahahahahahahahahahaha @samata"

Babu Tale "Jinsi nilivyokua naisubiria picha hii hata sitaki kusema sana zaidi ya kukupa hongera mtani kamwene baba @samagoal77 umefungua njia hapa naamini  inawezekana mwanangu @tamir_mrkucheka kuja kucheza majuu maana kupanga ni kuchagua #hainakufeli sasa Mr kimbunga @hamisi_kigwangalla usipepese macho tunaomba hii timu itangaze #TanzaniaUnforgettable sababu kuna mtanzania mwenzetu🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿"

Alikiba "Najiskia Furaha sana kukuona hapo ulipo @samagoal77 mwenyezi MUNGU akutangulie tuko nyuma yako kwa dua nzuri @asas_dairies @samakibafoundation #SupportedByKiba #KingKiba"

Proffesa J "Hongera sana CAPTAIN DIEGO @samagoal77 Sasa na sisi tunapata Heshima ya kuwa na Mwakilishi wa Nchi kwenye Moja kati ya Ligi Bora kabisa Duniani EPL, TANZANIA iko Pamoja na wewe, HAINA KUFELI💪🏻💪🏻

We Are PROUD of you ANKO @samagoal77"

Darassa "CHAMPION BOY 💪 @samagoal77 🙌🏻🙌🏻🙌🏻"

Jose Mara "Hongera sana champion 💪🏾💪🏾 @samagoal77 kwa hatua hii kubwa.. Kila la kheri inshaallah ☝🏾☝🏾☝🏾"

Nandy "VIVA SAMATTA 🇹🇿 congrat!!!! @samagoal77"

Mbosso "Mungu ni Mwema.. All The Best Bro  @samagoal77 #HainaKufeli"

Dude "Kila la kheri mzee🙏🙏 Ndiyo imetimia💪💪💪

@samagoal77"

Samatta atasalia Villa Park mpaka mwaka  2024 huku akitarajiwa kuwa mshambuliaji pekee ndani ya klabu hiyo inayopambana kubaki ligi kuu nchi Uingereza.

Baada ya kusaini mkataba huo ndani ya Villa, Samatta ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England.

Advertisement