Wachezaji Simba washerekea birthday ya Gadiel kwa kishindo -VIDEO

Thursday September 12 2019

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba wamesherekea pamoja siku ya kuzaliwa kwa beki Gadiel Michael baada ya kumaliza mazoezi yao ya asubuhi waliyofanya kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wachezaji hao walianza kwa kumbeba Gadiel na kumpeleka pembeni ya uwanja ambako walimwagia mchanga sambamba na maji ikiwa ni ishara ya furaha tu.

Katika tukio hilo, kiungo Msudani Sharaf Shiboub alimuonea huruma, kwa kumtafutia maji ili asafishe uso, lakini wachezaji wengine walimkataza na kusema aliwafanyia wenzie siku zilizopita.

Baada ya tukio hilo, walikata keki ambayo Gadiel aliandaliwa na jamaa zake kutoka nyumbani.

Tukio hilo limefanyika wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wao wa kesho Ijumaa wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Advertisement