Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tshishimbi Morrison, waingia anga za Eymael

Muktasari:

Kocha huyo raia wa Ubelgiji alisema ana matumaini Yanga itarejea kwa kishindo katika mechi za Ligi Kuu kwa kuwa anaridhika na kiwango cha kila mchezaji kwa namna anavyowafuatilia na kutoa maelekezo kwa njia ya mtandao.

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga Luc Eymael amesema wachezaji wanane akiwemo nahodha wake Papy Tshishimbi wanamnyima usingizi.

Eymael alisema tangu Ligi Kuu Tanzania Bara ilipositishwa kutokana na maambuzi ya ugonjwa wa corona amekuwa makini kufuatilia nyendo za wachezaji wanane Yanga.

Akizungumza na gazeti hili jana akiwa Ubelgiji aliwataja Lamine Moro, Bernard Morrison, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi, Said Juma ‘Makapu’, Patrick Sibomana na Tshishimbi.

Eymael alisema amekuwa makini na wachezaji hao kutokana na maelekezo ya kiufundi aliyoacha kwa wasaidizi wake wa benchi la ufundi baada ya mashindano kusimamishwa.

“Naomba nisieleweke vibaya kwamba nawafuatilia hawa tu, hapana nafuatilia wachezaji wote, lakini hawa wanane nataka kuona kama wanafuata kwa usahihi maelekezo ya benchi la ufundi

“Napenda kuona ubora wa viwango vyao unabaki kama nilivyowaacha kuanzia utimamu wa mwili haitapendeza nirudi niwakute baadhi ya wachezaji wameporomoka viwango vyao,”alisema Eymael.

Kocha huyo alisema kila siku amekuwa akipata ripoti ya wachezaji kupitia kwa wasaidizi wake Charles Mkwasa na Riedoh Berdien aliosema amekuwa akifanya nao kazi vizuri.

Alisema amekuwa akifutilia nyendo za kila mmoja kupitia kundi la timu kwa njia ya WhatsApp, video na simu za kawaida asubuhi na jioni ili kufahamu kila mchezaji anafanya nini na wakati gani.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji alisema ana matumaini Yanga itarejea kwa kishindo katika mechi za Ligi Kuu kwa kuwa anaridhika na kiwango cha kila mchezaji kwa namna anavyowafuatilia na kutoa maelekezo kwa njia ya mtandao.

Eymael alisema kwa namna ambavyo amekuwa akifuatilia nyendo zao ana imani hakutakuwa na mchezaji ambaye ataongezeka uzito na kushindwa kutoa mchango katika kikosi.

Alisema Yanga inatolea macho Kombe la FA ili kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho baada ya nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kuwa finyu kutokana na ubora wa Simba msimu huu.

Eymael alisema Yanga inatakiwa kufanya kazi ya ziada kupata tiketi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao. Simba na nafasi ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kufanya vyema katika mechi za mashindano hayo.

Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 nyuma ya Simba (71) na Azam (54) katika msimamo wa Ligi Kuu.