Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Tanzania yafuata kiungo Fountain Gate

JKT Pict

Muktasari:

  • JKT Tanzania tayari imejihakikishia nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kukusanya pointi 35 ikiwa nafasi ya sita kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 29, imeshinda minane, sare 11 na vipigo 10.

UONGOZI wa JKT Tanzania upo kwenye mazungumzo na kiungo wa Fountain Gate, Daniel Joram kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

JKT Tanzania tayari imejihakikishia nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kukusanya pointi 35 ikiwa nafasi ya sita kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 29, imeshinda minane, sare 11 na vipigo 10.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya JKT Tanzania, kimeliambia Mwanaspoti mazungumzo baina ya uongozi wa timu hiyo na mchezaji yapo kwenye hatua nzuri na wanaamini mambo yakienda vizuri dili litakamilika.

“Tayari tumeanza kuboresha kikosi chetu, hatuhitaji kuanza kupigana vikumbo na timu nyingine dirisha kubwa la usajili, hivyo naamini muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi ni wachezaji gani wapo mawindoni na wangapi tumemalizana nao,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza.

“Usajili unafanyika wakati wowote, masuala ya dirisha la usajili ni kukamilisha kile tulichokifanya kwa mazungumzo kwa kukiweka kwenye makaratasi na kusubiri uthibitisho.”

Mtoa taarifa huyo alisema msimu tayari umeshakamilika na ripoti ya mwalimu imekamilika, kilichobaki ni kuwakabidhi lakini wanafahamu ni nafasi gani zinahitajika kufanyiwa maboresho.

“Ubora wa kiungo huyo umetuvutia, tumemfuatilia kuanzia tulipocheza naye mchezo wa mzunguko wa kwanza na wa pili kocha alivutiwa na uwezo wake na kuagiza tuendelee kumpa jicho anaweza kutusaidia msimu ujao.

“Hicho kitu kimefanyika na tumeridhishwa na uwezo wake ukizingatia tulikuwa na uhitaji wa mchezaji wa aina yake kikosini kutokana na ripoti ya mwalimu,” alisema mtoa taarifa huyo.