Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twiga Stars yatwaa ubingwa CECAFA kwa rekodi za aina yake

Muktasari:

  • Twiga Stars itashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2024 yatakayofanyika Morocco kuanzia Julai 5 hadi Julai 26 mwaka huu.

Timu ya taifa ya soka ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imetwaa ubingwa wa mashindano ya Wanawake ya Baraza la vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kuichapa Kenya kwa bao 1-0 katika mechi ya mwisho ya mashindano hayo iliyochezwa leo kuanzia saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Twiga Stars imetwaa ubingwa huo huku ikiandika rekodi ya kutoruhusu bao lolote na yenyewe ikifumania nyavu mara 13 katika mechi nne.

Twiga Stars bingwa CECAFA 2025 ikiichapa Kenya
 
Bao pekee la ushindi la Twiga Stars lilikuwa la kujifunga la Enez Mango wa Kenya katika dakika ya 49 aliyekuwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake.

Ushindi huo umeifanya Twiga Stars ifikishe pointi 12 katika mechi nne ilizocheza na hivyo kujihakikishia taji huku Kenya ikimaliza katika nafasi ya pili na Uganda ipo nafasi ya tatu.

Twiga Stars ilianza mashindano hayo kwa kuichapa Sudan Kusini kwa mabao 4-0 kisha ikaifunga Burundi kwa mabao 6-0 na mchezo uliofuata ikaichapa Uganda kwa mabao 2-0 na ikaja kumalizia kwa ushindi huo dhidi ya Kenya.

Kocha wa timu ya taifa ya Wanawake ya Kenya, Berdine Odemba amesema kuwa Tanzania imekuwa kipimo kizuri kwao na amewapongeza kwa kutwaa ubingwa.

“Nawapongeza Tanzania kwa ushindi. Wameweza kutupa ushindani mzuri na wanaonekana wako tayari kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika.

“Kwetu mechi hii imetuonyesha vitu gani tunatakiwa kuvifanyia kazi kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu WAFCON,” amesema Odemba.

Kocha mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime amesema mashindano hayo yamekuwa na faida kwao.

“Tumeweza kuonyesha kiwango kizuri na tumeonyesha utayari. Niwapongeze Kenya wamekuwa kipimo kizuri kwetu,” amesema Shime.