Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lwasa mguu ndani, nje Kagera

LWASA Pict

Muktasari:

  • Lwasa raia wa Uganda, anaongoza kwa mabao katika kikosi cha Kagera Sugar na amefunga manane msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara, huku timu hiyo ikiwa imeshuka daraja na leo inakamilisha ratiba itakapocheza dhidi ya Simba.

NYOTA wa Kagera Sugar, Peter Lwasa mapema tu ana ofa mezani zinazomfanya kutokuwa na uhakika wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao itakaposhiriki Ligi ya Championship.

Lwasa raia wa Uganda, anaongoza kwa mabao katika kikosi cha Kagera Sugar na amefunga manane msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara, huku timu hiyo ikiwa imeshuka daraja na leo inakamilisha ratiba itakapocheza dhidi ya Simba.

Nyota huyo ambaye huu ni msimu wake wa kwanza ndani ya Kagera Sugar, amebakiza mkataba wa mwaka mmoja, hivyo kiwango alichoonesha baadhi ya timu zimevutiwa naye.

Taarifa kutoka Kagera Sugar ni, kutokana na uwepo wa ofa hizo, uongozi umeona kumuachia mchezaji kuamua hatma yake licha ya kwamba bado ina mkataba naye.

“Lwasa amecheza vizuri sana, katika wachezaji waliofanya vizuri licha ya kwamba timu imeshuka daraja yeye ni mmoja wao, bado tuna mkataba naye wa mwaka mmoja lakini ofa zilizopo zinaweza kumfanya akaondoka.

“Hivi tunavyoongea kuna ofa tulishazipokea na niseme wazi ni vigumu kumbakisha, ameshatuambia anaomba tuishie hapa na sisi tutafanyia kazi ofa zilizokuja kwetu,” alisema bosi mmoja wa Kagera Sugar.

Akizungumzia ishu hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu Kagera Sugar, Thabit Kandoro alisema mbali na Lwasa, kuna nyota wengine ambao wameanza kutolewa macho na timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara.

“Hayo yote, uamuzi wa mwisho tutaufanya baada ya ligi kumalizika, kwa sasa akili zote zipo kwenye mechi ya mwisho, kisha ndiyo tutaanza kuangalia nini kinachofuata,” alisema Kandoro.