Straika Mathare United afariki dunia

Monday August 17 2020
oliech pic

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Mathare United, Kevin Oliech amefariki dunia nchini Ujerumani alipokuwa anapatiwa matibabu ya saratani.

Msemaji wa familia, Nixon Onywanda amethibitisha kifo cha Kevin ambaye ni kaka wa nyota wa zamani wa Harambee Stars na klabu ya Gor Mahia, Dennis Oliech.

“Amekuwa akienda hospitali kupatiwa matibabu kwa miaka minne. Mwaka jana alirudi Kenya kisha akarejea Ujerumani ila kwa bahati mbaya tunasikitika tumempoteza,” amesema Onywanda

Mbali ya Mathare United timu nyingine alizowahi kuzichezea kwenye Ligi Kuu Kenya ni Nairobi City Stars, Tusker, Ushuru, na Defunct Securior.

Kifo chake kimekuja ikiwa ni miaka miwili imepita tangu mama yake, Mary Oliech afariki dunia, Julai 2018.

Advertisement