Nyota Bafana Bafana apania makubwa Afcon

Tuesday July 9 2019

 

By Eliya Solomon

Dar es Salaam. Nyota wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, Thulani Hlatshwayo ameweka wazi mpango wao katika fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ nchini Misri kuwa ni kufanya vizuri.

Thulani ni nahodha wa Bafana Bafana, alisema ushindi walioupata kwenye mchezo uliopita dhidi wa Misri ni kama ndio mwanzo hivyo uwa mengi mazuri yanakuja.

“Presha ni kubwa, lakini lengo letu ni moja tu kufanya vizuri kwenye fainali hizi, hatukuja kushiriki bali kushindana japo hatukuwa tukipewa nafasi. Vyovyote inatavyokuwa, huu kwetu ni mwanzo.

“Tunanafasi ya kufanya vizuri zaidi ili kuacha historia, naamini kizazi hiki kinauwezo wa kufanya chochote kwa yeyote,” alisema mchezaji huyo nahodha wa Bidvest Wits.

Bafana Bafana iliwashangaza wenye kwenye AFCON katika hatua ya 16 ambapo waliwang’oa wenyeji wa fainali hizo, Misri kwa kuwafunga bao 1-0, kesho  watakuwa na kibarua cha kucheza na Nigeria.

Advertisement