Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunifu Zampolini wa Italia kupamba Swahili Fashion weeks

Muktasari:

Mbunifu wa mavazi wa Italia anatarajiwa kupamba wiki ya ubunifu ya Swahili inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 6

Dar es Salaam.Onyesho la ubunifuni wa mavazi la Swahili Fashion Week litafanyika Desemba 6 hadi Desemba 8, likimshirikisha mbunifu maarufu kutoka Italia, Marta Zampolini.

Akizungumza leo Novemba 18, 2019 Mratibu wa shindano hilo, Mustafa Hassanali amesema mwanamitindo huyo wa Italia atatoa mafunzo kwa wanamitindo hapa nchini namna ya kuzitengeneza bidhaa zao katika mfumo ambao utazifanya bidhaa zai ziuzike nje ya nchi.

Kuhusu onyesho la mwaka huu amesema litausisha wanamitindo 34 kutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema wanasaka wanamitindo wenye muonekano makini kwa ajili ya kuonyesha mitindo ya mavazi katika jukwaa la Swahili Fashion Week kwa mwaka huu, litafanyika Novemba 24.

Vigezo wa wanamitindo hao ni urefu usiopungua sentimita 172 bila viatu virefu kwa wanawake na, sentimita zisizopungua 180 kwa mwanaume ikiwa ni pamoja na muonekano wa kuvutia.

Hassanali alisema mwaka huu kutakua na tuzo maalum kwa wabunifu kutoka mkoani ili kuwapa fursa na kuwatambulisha kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi.

Naye Rais wa  Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Adrian Nyangamale amesema jukwaa la Swahili Fashion week ni kiunganishi kwa nchi zinazoongea Kiswahili lengo likiwa ni kuikuza lugha hiyo na pia kujitangaza zaidi kimataifa kuelekea uchumi wa Kati.