VIDEO: Katwila, Mziba wajumuishwa Kilimanjaro Stars, Nado aumia

Muktasari:

Katwila aliingoza timu za vijana za taifa U-20, kutwaa ubingwa atakuwa kocha msaidizi pamoja na Selemani Matola huku Mzima akiwa meneja wa timu hiyo.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubeir Katwila na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Abeid Mziba wamejumuishwa katika benchi la ufundi la timu ya Taifa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kinachojindaa na mashindano ya Chalenji, Uganda.

Katwila aliingoza timu za vijana za taifa U-20, kutwaa ubingwa atakuwa kocha msaidizi pamoja na Selemani Matola huku Mzima akiwa meneja wa timu hiyo.

Kilimanjaro Stars itakuwa chini ya kocha mkuu Juma Mgunda, huku Mrundi Étienne Ndayiragije atakuwa na jukumu la kuangalia timu zote mbili za Tanzania bara na Visiwani.

Pia, kuna uwezekano Matola asiende Uganda kutokana na kuwepo kwa taarifa za kujiunga na Simba.

Idd Nado ashindwa kufanya mazoezi

Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, Seleman Idd 'Nado' ameshindwa kufanya mazoezi na timu leo Jumanne kutokana na maumivu ya mguu.

 

Nado anayechezea Klabu ya Azam FC, amekaa nje ya uwanja na kuwa mtazamaji kwa sababu ya maumivu hayo ambapo sehemu ya juu ya kanyagio cha mguu wake wa kulia inaonekana imevimba kidogo.

"Nipo tu hapa napumzika, nina maumivu kidogo ya mguu ndio maana nipo nipo tu," alisema Nado.

Kilimanjaro Stars inaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.