Hakimu Mkazi, Kasonde kusoma hukumu kesi Malinzi leo

Muktasari:

Kesi hiyo ya jinai namba 213/2017 washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha

Dar es Salaam. Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake inatarajiwa kutolewa hukumu leo Jumatano Desemba 11, 2019 na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Hakimu Kasonde aliyekuwa Hakimu Mkazi Kisutu kwa sasa amehamishwa ndiye anatajiwa kusoma hukumu hiyo.

Washtakiwa hao kama ilivyo kawaida wamefika mahakamani hapo tangu asubuhi na kuwekwa eneo wanalohifadhiwa washtakiwa wakisubilia kesi zao kutajwa.

Watu mbalimbali wakiwemo ndugu wa washtakiwa hao wamefika mahakamani hapo wakisubilia hukumu hiyo.

Mbali na Malinzi wengine ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya

Kesi hiyo ya jinai namba 213/2017 washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335.