Bao la Fati wa Barcelona lavunja rekodi ya miaka 22 Ligi ya Mabingwa

Wednesday December 11 2019

Mwanaspoti-Bao-Fati-Barcelona-lavunja-rekodi-miaka 22-Ligi ya Mabingwa

 

Milan, Italia. Chipukizi Barcelona, Ansu Fati amekuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga bao katika historia ya Ligi ya Mabingwa akivunja rekodi ya miaka 22 iliyowekwa na Peter Ofori-Quaye.

Chipukizi Fati akiwa na miaka 17 na siku 40 alifunga bao la ushindi la Barcelona lililoiondoa Inter Milan katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa.

Kabla ya bao la Fati kwenye uwanja wa San Siro usiku wa jana aliyekuwa akishikiria rekodi ya kufunga bao akiwa mdogo zaidi ni Peter Ofori-Quaye aliyeifungia Olympiacos dhidi ya Rosenborg msimu wa 1997-98.

Ofori-Quaye alikuwa na miaka 17 na siku 194, wakati alipofunga bao lake katika mechi ya hatua ya makundi iliyochezwa Oktoba 1997.

Ni rekodi nyingine nzuri kwa Fati aliyoandika baada ya mwanzoni mwa msimu huu kuwa mchezaji mdogo zaidi kuifungua Barcelona.

Pia, amekuwa mchezaji wa tatu mdogo kufuga katika La Liga baada ya kufunga bao katika mechi ambayo Barcelona ililazimishwa sare 2-2 na Osasuna mwezi Agosti.

Advertisement

Bao lake alililofunga San Siro limekuwa ni muhimu zaidi kwa sababu limeipa ushindi Barca ikiwa ni muda mfupi baada ya Carles Perez kufunga bao dakika 85.

Wakiingia kutoka benchi Fati alishirikiana vema na Luis Suarez kabla ya kupiga shuti lililojaa wavuni.

“Nilicheza kwa kugongeana pasi na Luis nilipofunga uwanja wote ulikuwa kimya. Nimefurahi sana!” alisema Fati.

“Ni ndoto. Kila kitu kinakwenda kwa kasi. Natumia kila nafasi ninayopewa. Lakini ukigeuka na kuangalia na kufikiri: "Nini nilichokifanya"?'

Advertisement