Moyes ampigania Ole Man United

Muktasari:

Ukiachana na Moyes, makocha wengine waliopita Man United tangu kuondoka kwa Alex Ferguson ni Louis van Gaal na Jose Mourinho.

LONDON, England .KOCHA wa zamani Manchester United David Moyes kaibuka na kusema kuwa hakuna sababu ya kumzodoa  Ole Gunnar Solskjaer kwani anaamini atapata mafanikio katika klabu yake msimu huu.

Kocha huyo raia wa Scotland ameenda mbele na kuwataka mashabiki kuwa watulivu na kumpa nafasi Ole ili afanye yake.

  “Ni kazi ngumu, kila mtu ameona namna shughuli hiyo ilivyo, mimi nilishindwa, Louis van Gaal na Jose Mourinho nao walishindwa. Ukiangalia kwa makini utaona kwamba makocha walioshindwa kufanya vizuri pale ni wazoefu sana.  

“Utakuwa msimu mwingine mgumu kwa Ole, lakini nadhani anafanya kila liwezekanalo ili mambo yaende sawa. Naamini atafanikiwa. Hata hivyo watu wana matarajio makubwa kutoka kwake. Wanatakiwa kuwa na uvumilivu.

“Unapokuwa kocha wa Man United watu wanategemea kuona unashinda kila mechi. Na vile vile kila unaposhinda mechi unatakiwa ushinde kwa kishindo au kwa mtindo mzuri wa kuwafurahisha mashabiki.

“Ole anafahamu hilo na ndio maana anatakiwa kujitahidi 

“Wamejaribu kusaini wachezaji chipukizi ili wawakuze kwa ajili ya mafanikio ya karibu na ya baadaye. Nakumbuka waliwahi kumsajili Wayne Rooney kutoka kwetu (Everton) akiwa na miaka 18 tu, baadaye alikuwa bora sana. Nadhani hata mpango huo utawasaidia.