Mourinho ajitetea kwa Alli

Tuesday September 15 2020

 

London, England. Kocha Jose Mourinho amesisitiza kuwa uamuzi wake wa kumtoa Dele Alli ulikuwa wa kiufundi na kuwashutumu wachezaji wake kwa kuwa na ‘uzembe’ uwanjani.

Spurs ilichapwa bai 1-0 na Everton katika mchezo wao wa kwanza wa msimu mpya wa Ligi Kuu England uliofanyika juzi usiku.

Mourinho aliwakera mashabiki kwa kumtoa Alli baada ya dakika 45 za kwanza, kabla ya Dominic Calvert-Lewin kufunga bao la ushindi dakika ya 55.

Ilionekana kuwa kiwango cha Moussa Sissoko hakikuwa bora na ndiye ambaye alistahili kutoka, lakini haikuwa hivyo kwa kocha huyo.

Lakini baada ya mchezo huo kumalizika, Mourinho alisisitiza kuwa uamuzi wake katika mchezo huo ulikuwa katika mbinu za kiufundi.

Kocha huyo wa kireno aliuambia mtandao wa Sky Sports: “Ndiyo, ni kiufundi. Walikuwa wakicheza kwa kutumia winga mmoja, Allan alikuwa katika upande mmoja.

Advertisement

“Gomes na Doucoure walikuwa wakisukuma vizuri mashambulizi, kulikuwa na nafasi kubwa iliyokuwa wazi. Nilihitaji wawe na uwezo zaidi ya pale katyika kuziba nafasi.”

Mourinho alionekana mara mbili akimuita Alli ‘mzembe’ katika vipindi vya runinga vya Spurs (fly-on-the-wall All Or Nothing).

Kocha huyo wa Spurs pia aliwashukia wahssmabuliaji wake kutokana na kile alichokiita kuwa na presha na kukosa utulivu katika eneo la mwisho kwenye mchezo wa juzi.

Alisema: “Tulikuwa wazembe katika kushambulia. Hayo nimatokeo ya kutokuwa fiti, muda mbaya wa kuandaa timu. Kuna wachezaji hata hawakuwepo wakati wa maandalizi ya mwanzo wa msimu.

 

Advertisement