Mkongwe Oliech adai Gor Mahia ni hafifu mno msimu huu

Thursday November 7 2019

Mkongwe -Oliech -adai -Gor Mahia - hafifu- msimu-Kogalo -Dennis-

 

Nairobi, Kenya. STRAIKA wa zamani wa Gor Mahia, aliyetemwa na klabu hiyo, Dennis Oliech kadai Kogalo hawako kabisa msimu huu.

Akifunguka kuhusu utathmini wake wa ushindani wa Gor baada yao kubanduliwa kwenye dimba la CAF Confederation juzi Jumpili, Oliech kadai Kogalo hawawezani kabisa msimu huu.

Oliech anayetajwa mmoja kati ya mastraika bora kuwahi kutokea Kenya, anasema kikosi cha sasa cha Gor ni hafifu mno kumtishia yeyote.

Ijapo wanakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya KPL kwa sasa kwakiwa na mechi mbili za viporo, bado Oliech hana imani na uboraa wa kikosi hicho.

Kasisitiza matokeo bora wanayoweza kusajili msimu huu kwenye ligi ni kumaliza katika nafasi ya tatu. Hii ikiwa ni baada yao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu mfululizo katika misimu iliyopita.

“Ndio Gor Mahia wameanza ligi msimu huu kwa vishindo lakini rekodi zao za mechi za ugenini ni mbovu na ndio sababu sioni wakibeba ubingwa wa ligi safari hii. Matokeo bora wanayoweza kusajili msimu huu ni kumaliza katika nafasi ya tatu au nne. Waliuza sana wachezaji wazuri na wazoefu mwishoni mwa msimu uliopita na wale walipo kwa sasa bado wanahitaji muda ili waweze kujeli vizuri,” Oliech kafafanua.

Advertisement

Miongoni mwa wachezaji mahiri waliogura timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita ni pamoja na beki kisiki aliyekuwa nahodha wao Harun Shakava, kiungo fundi Francis Kahata, mastraika Meddie Kagere na Jacques Tuyisenge.

Jumapili Gor walibanduliwa nje ya dimba la CAF na Wacongo DC Motema Pembe, ikiwa ni mara yao ya kwanza kushindwa kufuzu kwa hatua ya makundi ya dimba l hilo la CAF Confederation katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita na sasa wanajiandaa na mchezo wa Mashemeji Derby utakaopigwa Jumapili.

Advertisement