Mkenya aandika historia ya mbio za marathoni duniani

Saturday October 12 2019

 

Mwanariadha wa Kenya, Elliud Kipchoge amefanikiwa kumaliza mbio za marathoni kwa kutumia muda wa chini ya saa mbili.
Akiwa amevalia jezi nyeupe na kusaidiwa na wanariadha saba wa kumuongezea kasi (pace makers), Kipchoge, ambaye ni bingwa wa dunia na Olimpiki wa marathoni, alipita barabarani akiwa anashangiliwa.

Alianzia darajani na kumalizia kwenye bustani ya Prater na kuweka rekodi ya dunia.

Advertisement