Kipchoge aweka rekodi mpya London Marathon

Muktasari:

Zaidi ya wanariadha 40,000 walishiriki mbio hizo ambazo zimekusanya zaidi ya pauni 1 bilioni

Arusha. Mwanariadha Bingwa wa dunia Mkenya Eliud Kipchoge amezidi kutengeneza rekodi nyingine baada ya kushinda mbio London Marathon akitumia muda was aa 2:02: 38.

Katika mbio hizo Kipchoge ametetea taji lake kwa mara ya nne akitengeneza rekodi mpya baada ya kumaliza wa kwanza akitumia saa 2:02:38, akifuatiwa na Mule Wasihuh aliyemaliza wa pili kwa saa 2:03:16 na nafasi ya tatu ikienda kwa Bashir Abdi 2:07:03.

Kwa upande wa wasichana nafasi zote tatu za juu zimechukuliwa na wanariadha kutoka Kenya wakiongozwa na Brigid Kosgei aliyekata utepe kwa saa 2:18:20, akifuatiwa na Vivia Cheruiyot kwa saa 2:20:14 huku nafasi ya tatu akishikwa na Rosa Dereje aliyemaliza kwa saa 2:20:51