Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fadlu ashikilia faili la kiungo Mkongo

FADLU Pict
FADLU Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo aliyepo mapumziko kwa sasa, ndiye anayesubiriwa kufanya maamuzi ya kusajili wa kiungo huyo aliyewahi kuhusishwa na Yanga na kuonekana kama angetua Jangwani ili kuungana na pacha wake, Maxi Nzengeli aliyewahi kucheza naye wakiwa kwao DR Congo.

KIKOSI cha Simba kinaendelea kupiga hesabu ya kuingiza mashine mpya na kuzitema zile ambazo hazina mipango nayo kwa msimu ujao, lakini kuna kiungo mshambuliaji mmoja kutoka DR Congo ambaye faili lake limetua mezani mwa kocha Fadlu Davids.


Kocha huyo aliyepo mapumziko kwa sasa, ndiye anayesubiriwa kufanya maamuzi ya kusajili wa kiungo huyo aliyewahi kuhusishwa na Yanga na kuonekana kama angetua Jangwani ili kuungana na pacha wake, Maxi Nzengeli aliyewahi kucheza naye wakiwa kwao DR Congo.


Ipo hivi. Kocha Mkuu wa  Simba, Fadlu Davids imeelezwa ndiye aliyeshikilia hatma ya usajili wa kiungo mshambuliaji, Âgée Basiala Amongo (26) anayetokea klabu ya AS Maniema Union ya DR Congo ili aone kama atahitaji huduma yake msimu ujao.

Chanzo cha ndani kutoka Simba kinasema viongozi wa klabu na wasimamizi wa mchezaji huyo, wamefanya mazungumzo na kufikia pazuri, lakini mwenye maamuzi ya mwisho ni kocha Fadlu wanayemsubiri atoke mapumziko akirejea wafanye naye kikao.

"Kama viongozi tumeona ni mchezaji mzuri, lakini lazima kocha atoe maamuzi ya mwisho na sio huyo pekee, wapo wengine tuliozungumza nao, lakini bado hawajasainiwa," kilisema chanzo hicho na kuongeza;

"Kama kocha alipendekeza wachezaji baadhi ambao bado wana mkataba, lakini tumejaribu kuangalia plani B ya nafasi zilezile, ndio maana tunataka akija ili apitie wasifu wa akiona wanafaa tutachukua hatua ya utelekezaji."

Endapo usajili wa Basiala ukikamilika atakuwa na kibarua cha kupambania namba mbele ya kinara wa mabao 16 Ligi Kuu iliyoisha, Jean Charles Ahoua aliyemaliza na asisti tisa, alicheza mechi 28, dakika 2098, wakati Awesu Awesu alicheza mechi 19, alifunga bao moja, asisti moja na dakika 776.

Mwanaspoti awali liliandikla kwamba Yanga ndio ilikuwa klabu ya kwanza kuhitaji huduma yake, ili kutaka kuwaunganisha tena na Maxi Nzengeli waliwahi kucheza pamoja wakiwa DR Congo kabla ya mazungumzo kuishia njiani na Simba kuingilia kati na kufanikiwa kushawishi menejimenti yake ili atue Msimbazi kwa msimu ujao wa mashindano ambapo Simba itashiriki pia Ligi ya Mabingwa Afrika.