Kipchonge atamani rekodi ya kutukuka Berlin Marathon

Friday September 15 2017

 

By Na Thomas Matiko

Mkali wa Marathon, Eliud Kipchoge anayejiandaa kwa Berlin Marathon Septemba 24 nchini Ujerumani ikiwa ni wiki moja kutoka sasa, amesema anataka historia imkumbuke kama Floyd Mayweather.
Bondia Mayweather alichapana ngumi zake za mwisho mwezi uliopita  dhidi ya Conon McGregor na kumshinda kwa KO iliyomhakikishia rekodi yake inasimama kwa mapambano 50-0 huku akiwa hajawahi kupoteza  pambano hata moja.
Ni rekodi ambayo imemweka katika vitabu vya kumbukumbu vya ndondi na vilevile kumwingiza katika hadhi ya ‘Hall of Fame’ ambayo hujumulisha majina ya mastaa wakali wastaafu waliaocha rekodi ya kusifiwa kwenye fani ya mchezo.
Hadi kufikia sasa, Kipchoge kashiriki Marathon nane tangu 2013 alipojitosa kwa mara ya kwanza kwenye Hamburg Marathon na kama rekodi yake inaweza kuandikwa kama ya wanabondia, basi itasimama kwa 7-1 kwani maana kuwa amepoteza mara moja.
 Kipchoge ameshinda Marathon saba katika taaluma yake  isipokuwa moja ile ya Berlin Marathon 2013 alikomaliza wa pili nyuma ya Wilson Kipsang  ambaye atakuwa mpinzani wake tena wikendi ijayo.

Advertisement