Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msimu umeisha, boresheni viwanja sasa

MSIMU Pict

Muktasari:

  • Viongozi wa timu na maofisa wa mabenchi ya ufundi, wanakitumia kipindi hiki kuboresha vikosi vyao kwa kuwaondoa baadhi ya wachezaji ambao wanaonekana hawawezi kuwa na mchango mkubwa kwa timu na kuingiza wale ambao wanahisi wataimarisha vikosi.

MSIMU unapomalizika, ni fursa nzuri kwa wachezaji kupumzisha miili baada ya kuitumikisha kwa zaidi ya miezi nane kama sehemu ya kuwajibika kwa timu zilizowaajiri.

Viongozi wa timu na maofisa wa mabenchi ya ufundi, wanakitumia kipindi hiki kuboresha vikosi vyao kwa kuwaondoa baadhi ya wachezaji ambao wanaonekana hawawezi kuwa na mchango mkubwa kwa timu na kuingiza wale ambao wanahisi wataimarisha vikosi.

Mamlaka za soka nazo hutumia kipindi hiki kufanya tathmini ya maeneo gani ya kuyaimarisha na vitu gani vya kuviondoa ili msimu unaofuata uwe bora na wenye mvuto zaidi.

Hata hivyo, kijiwe kinakumbusha jambo moja la msingi ambalo linapaswa kufanywa katika kipindi hiki cha mapumziko ambalo ni maboresho  ya viwanja ambavyo tunategemea vitatumika kwa Ligi Kuu msimu unaofuata.

Uwanja wa soka ni jambo la muhimu sana katika mchezo wa mpira wa miguu na ndiyo maana umepewa kipaumbele katika sheria 17 za mchezo huo kwani ndiyo sheria namba moja na ni sahihi maana bila uwanja hakuna kinachoweza kufanyika.

Kwa msimu uliomalizika, kasoro kubwa ya baadhi ya viwanja ilikuwa ni katika eneo la kuchezea ambapo katika viwanja vingi, hali haikuwa nzuri na kusababisha mechi zisichezeke vyema.

Maeneo ya kuchezea ya viwanja yanapokuwa katika ubora wa hali ya juu, yanasaidia timu kufanyia vyema kazi mbinu na mipango ya makocha wao,  pia wachezaji kuonyesha ufundi walionao kinyume na pale wanapocheza katika viwanja ambavyo havina eneo zuri la kuchezea.

Pia uboreshaji viwanja unapaswa kufanyika katika maeneo mengine kama vile vyumba vya kubadilishia nguo, majukwaa ya mashabiki na vyumba vingine vya maofisa wa mchezo.

Kwa vile kutakuwa na muda mrefu kabla ya ligi kurejea, ukarabati wa viwanja unapaswa kufanywa katika kipindi hiki na siyo kungojea kufanya wakati tayari msimu mpya ukiwa umeshaanza.