Olimpiki 2020 mtihani kwa Kipchoge

Thursday April 18 2019

 

 

MAKALA ya Olimpiki zijazo zitakazoandaliwa Tokyo 2020 zimenukia na sasa wataalamu wa afya wametoa tahadhari kwa staa, Eliud Kipchoge na wanariadha wenzake waliopanga kushiriki kwenye Marathon ya makala hayo.

 Makala ya 2020 ya mashindano hayo ambayo huja kila baada ya miaka minne, hilo limeratibiwa kuandaliwa kati ya Julai 24 na kufululiza hadi Agosti 9 yatakapofikia kikomo. Kipindi hiki, kitakuwa ni majira ya joto kule Tokyo.

Baada ya kushauriwa na wataalamu wa afya kuwa vitengo vinavyohusisha mbio ndefu huenda vikakumbwa na majanga ya kiafya kutokana na joto kali, waandalizi wameamua kubadilisha ratiba ya mbio hizo na kuzihamishia masaa ya alfajiri.

 Mbio za Marathon sasa zitaanza saa 12 alfajiri kwa majira ya Japan (saa sita mchana kwa majira ya Afrika Mashariki) huku zile za kutembea umbali wa kilomita 50, zikianza saa 11 unusu alfajiri.

“Uamuzi huu umechukuliwa ili kuweza kulinda afya za wanariadha kutokana na hali ya joto kali msimu huo,” alisema Mwandalizi Koji Murofushi.

Advertisement

 Kwa kawaida mbio za Marathon kote ulimwengu huandaliwa kati ya saa tano asubuhi au saa saba mchana hivyo kwa madailiko haya, wanariadha watalazimika kuzoeasha miiili yao kuingiliana na hali hii.

Advertisement