Mavoko wampokonya MTC ubingwa

Timu ya Mavoko ndio mabingwa wapya wa michuano ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere cup yaliyomalizika mkoani Arusha.

 

Mavoko imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kumchapa bingwa mtetezi wa kombe  hilo timu ya MTC ya Mwanza kwa jumla ya seti 3-0.

 

Mashindano hayo ya wavu ya kimataifa yaliyochezwa katika viwanja vya Ngarenaro, yalishirikisha jumla ya timu 17 zikiwemo 11 za wanaume na sita za wanawake.

 

Akizungumzia ubingwa wao nahodha wa timu ya Mavoko, Ngeny alisema wamefurahi ubingwa huo na wanaahidi kuutetea tena mwakani.

 

Nahodha wa timu ya MTC David Neeke alisema wamesikitika kupoteza ubingwa wao lakini haiwavunji moyo kwani ugumu wa mashindano ndiyo yaliyopelekea hayo na wanaahidi kupata maandalizi ya mapema msimu ujao.

Kabla ya mchezo huo timu hizo zilitambiana kwa tambo za aina mbalimbali.

Timu ya Mavoko inacheza fainali baada ya kuiondoa timu ya Rukinzo ya Burundi kwa seti 3-0 huku timu ya MTC ikipata nafasi hiyo baada ya kuitoa timu ya Arusha champion kwa seti 3-1.

Nahodha wa Mavoko Sammy Ngeny alisema kuwa mchezo huo utakuwa na burudani ya aina yake kutokana na maandalizi waliyoyafanya ya kuutaka ubingwa.

"Nawaonea huruma MTC maana wataingia wakidhani wanakutana na timu zembe, lakini wajue tu kuwa wajipange wawezavyo lakini ubingwa tunauchukua wakiona"

Nae kocha wa MTC, Safari Yabunika alisema kuwa ameshajipanga kuwavaa Mavomo tangu walipogundua kuwa ndio wapinzani wao katika mchezo wa Fainali hiyo hawatakuwa na muda wa kupoteza kwao zaidi ya kuuttetea ubingwa wao.

"Mavoko si timu ngeni kwani nimeona michezo yao yote waliyocheza tangu kuanza  mashindano hivyo hawana cha kunitisha ingawa ni timu nzuri iliyofanikiwa kuleta ushindani wa hali ya juu"