Man United kwa Chelsea, Liverpool, Arsenal, Man City waanza na vibonde

Thursday June 13 2019

 

London, England. Mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City itaanza kutetea ubingwa wake dhidi ya West Ham wakati Manchester United itafungua ligi dhidi ya Chelsea Agosti 11 katika msimu wa 2019-20.

Katika ratiba hiyo ya Ligi Kuu England iliyotolewa leo inayonyesha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool watafungua msimu nyumbani dhidi ya timu iliyopanda daraja la Norwich City hapo Ijumaa ya Agosti 9.

Mabingwa Manchester City watakuwa ugenini Agosti 10 kuifuata West Ham. Timu zilizopanda daraja za Aston Villa na Sheffield United watakata utepe kwa kucheza dhidi ya Tottenham na Bournemouth.

Jumapili ya Agosti 11, Manchester United watakuwa nyumbani kuwakaribisha Chelsea.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England, klabu zitapata mapumziko mafupi ya wiki mbili mwezi Februari.

Mapumziko hayo katika wiki ya kwanza kutakuwa na mechi tano na wiki ya pili mechi tano ili kuhakikisha kila klabu inapata wiki moja ya kupumzika.

Advertisement

Ngao ya jamii

Mechi ya ufunguzi wa msimu ya Ngao ya jamii itawakutanisha Liverpool dhidi ya Manchester City kwenye Uwanja wa Wembley siku ya Jumapili Agosti 4.

Liverpool na mabingwa wa Europa Ligi, Chelsea pia watakutana katika Uefa Super Cup jijini Istanbul, Uturuki, Jumatano ya Agosti 14.

Baada ya mechi hiyo, Liverpool itacheza mechi ya pili ya Ligi Kuu ugenini dhidi ya Southampton, wakati Chelsea itawakaribisha Leicester City.

Wolves inatakiwa kucheza mechi tatu za kusaka kufuzu kwa Europa Ligi kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England.

Ratiba ya ufunguzi

9 Agosti 2019       Liverpool v Norwich City    

10 Agosti 2019     West Ham v Manchester City

10 Agosti 2019     Bournemouth v Sheffield United     

10 Agosti 2019     Burnley v Southampton

10 Agosti 2019     Crystal Palace v Everton

10 Agosti 2019     Leicester City v Wolves

10 Agosti 2019     Watford v Brighton

10 Agosti 2019     Tottenham v Aston Villa    

11 Agosti 2019     Newcastle United v Arsenal      

11 Agosti 2019     Manchester United v Chelsea 

Advertisement