Makambo akutana na balaa la ‘wajeda’ Ruvu Shooting, apigwa roba uwanjani

Wednesday May 15 2019

 

By Michael Matemanga

Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo akutana na balaa la Ruvu Shooting katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Heritier Makambo alikutana na balaa la kuandamwa na wachezaji wa Ruvu Shooting kwa kuanza kuchezewa mpira wa kibabe baada ya kumpiga kipepsi beki, Santos Mazengo na kumsababishia kutoka damu.

Baada ya tukio ilo wachezaji wa Ruvu shooting walilalamika kwa mwamuzi wakimtaka apewe kadi, hata ivyo mwamuzi hakutoa kadi hali iliyoamsha hasira kwa wachezaji wa Ruvu Shooting.

Moja ya balaa alilokutana nalo Heritier Makambo ni pale alipopigwa roba na beki wa Ruvu Shooting, George Amani huku akiwa hana mpira wakati mechi ikiendelea.

Katika mechi hiyo Yanga iliibuka na ushindi wa bao moja, bao ambalo lilifungwa na Papy Tshishimbi na kuwafanya kufikisha pointi 83 baada ya kucheza mechi 36 huku watani wao wakibakiwa na pointi 82 baada ya kucheza mechi 33.

Advertisement