Kotei asaini miaka mitatu Kaizer Chief, aitupia lawama Simba

Wednesday June 26 2019

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Kiungo wa Simba, James Kotei amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea Kaizer Chief ya Afrika Kusini.

Klabu ya Kaizer Chiefs imemtambulisha Kotei kupitia akaunti Twitters ikisema imefanikiwa kumnasa Mghana huyo akiwa mchezaji huru kutoka Simba.

Akizungumzia sakata la kuondoka Simba, Kotei kiungo bora wa mwaka wa Simba alisema kabla ya mkataba wake na Simba kumalizika aliwasiliana na viongozi wa timu yake akiwakumbusha suala hilo kutoka alikuwa na ofa za timu mbalimbali zilikuwa zikitaka saini yake mara baada ya mkataba kufikia ukingoni.

"Wakati naendelea kusubiri uamuzi yao na niliwaeleka wazi kuna timu nyingi zilikuwa zikitaka saini yangu niliwaeleza kuwa natakiwa na timu nyingi kutoka nyumbani Ghana, Afrika Kusini na nchi nyingine, lakini hawakuonesha nia ya kujali hilo," alisema Kotei.

"Niliwapa nafasi kubwa na kipaumbele timu yangu ya Simba, lakini hawakuonesha heshima kwangu wakaamuaa kuachana nami na nilikuwa sina jinsi kutafuta timu nyingine kwani mpira ndio kazi yangu," alisema Kotei.

"Kimsingi nimemalizana na Kaizer Chiefs, lakini nilifanya hivi baada ya Simba kushindwa kuonesha heshima yao kwangu kutokana na kazi ambayo nimeifanya katika timu hiyo kwa miaka yote niliyocheza hapo," aliongezea Kotei.

Advertisement

Advertisement