Fei Toto: Nikirudi nitakuwa mkali zaidi

Wednesday March 25 2020

Fei Toto: Nikirudi nitakuwa mkali zaidi,Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ,ugonjwa wa corona,

 

By Olipa Assa

Dar es Salaam. Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema hana wasiwasi na kiwango chake ligi itakapoanza atakuwa bora zaidi.

Fei Toto amesema akicheza anakuwa anajisikia burudani kwa kuwa anapenda soka ndio jambo linalomwaminisha hatayumba kiuwezo.

"Kipaji cha mtu hakiwezi kuyumbishwa kwa namna yoyote ile labda aumwe, ugonjwa wa corona tunaambiwa namna ya kujikinga hivyo hauwezi kuzuia kufanya mazoezi."

"Siwezi kujisikia raha bila kufanya mazoezi kwa sababu nakuwa nahisi kama napungukiwa, kikubwa ni mchezaji mmoja mmoja kujitambua basi," amesema Fei Toto.

Fei Toto amesisitiza anaendelea kufanya mazoezi ya gym na kukimbia kuhakikisha akirejea kazi anakuwa katika kiwango cha juu.

Advertisement