Diamond, Pari Match kumleta Mike Tyson Tanzania

Thursday September 12 2019

 

By Imani Makongoro na Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platinum na Kampuni ya Pari Match Tanzania iko mbioni kumleta nchini bingwa wa zamani ngumi wa dunia wa uzani wa juu, Mike 'Iron' Tyson.

Akizungumzia ujio wa Tyson, Diamond alisema atawasili nchini hivi karibu.

"Nimezungumza naye, yuko tayari na siku si nyingi tutaweka wazi lini atawasili," alisema Diamond mara baada ya kutambulishwa rasmi kuwa balozi wa Pari Match Tanzania jijini Dar es Salasm.

Mkurugenzi Mtendaji wa Pari Match Tanzania, Tumaini Maligana amesema Mike Tyson ni miongoni mwa mabalozi wa kampuni hiyo atakuja nchini kwa mapumziko mafupi.

"Atashirikiana na Diamond katika kuwafundisha watu njia bora ya kucheza kwa kubashiri matokeo na nafasi ya Pari Match katika mchezo wa kubashiri ambapo kwetu ni kama burudani si ajira,” alisema Maligana.

Advertisement