Coutinho kurudi Anfield ngumu sana

Friday February 14 2020

Coutinho kurudi Anfield ngumu sana,STAA wa Kibrazili, Philippe Coutinho ,Liverpool,Anfield ,Barcelona,

 

LIVERPOOL,ENGLAND. STAA wa Kibrazili, Philippe Coutinho ameripotiwa kwamba ana nafasi ndogo ya kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya Liverpool baada ya kuwapo kwa taarifa ndani ya wiki hii huenda akarudi zake Anfield mwisho wa msimu.

Coutinho anaonekana kuwa hana lake tena Barcelona ikiwa ni miaka miwili tu imepita tangu aliponaswa kwa mkwanja wa Pauni 142 milioni kutokea Liverpool.

Kwa sasa staa huyo yupo kwa mkopo Bayern Munich, lakini miamba hiyo ya Bundesliga haina mpango wa kumchukua moja kwa moja, jambo ambalo litafichua kwamba atalazimika kutafuta timu mpya itakapofika mwisho wa msimu huu.

Liverpool inahusishwa, lakini jambo hilo halionekani kuwa na uwezekano wa kutokea. Kocha Jurgen Klopp alimwonya Coutinho mwaka 2017 asiondoke, lakini Januari ya mwaka uliofuatia tu, aliondoka zake kwenda Barcelona.

Coutinho alipuuzia akasepa.

Advertisement