Beki Simba hana presha

Muktasari:

  • Miraji ni miongoni mwa wachezaji walioibuliwa katika kikosi cha vijana cha Simba kuanzia mwaka 2011 kilichokuwa chini ya Seleman Matola.

BEKI  wa zamani wa Simba, Miraji Adam ametamba kuwa  kukaa kwake nje kwa muda mrefu hakutokuwa sababu ya kumfanya aanze upya pindi akirejea uwanjani.

Miraji msimu huu alisajiliwa na Ndanda Fc lakini baadaye alijiondoa katika kikosi hiko na kukaa pembeni na tangu hapo hajachezea wala kusajiliwa na timu nyingine yoyote.

Akizungumza na Mwanaspoti, Miraji alisema licha ya kutokuwa na timu anaamini katika mazoezi yake anayofanya.

"Siwezi kupotea kama nitafuata misingi mizuri basi naamini nitarudi na kuendelea pale nilipoishia kwac sababu naamini wachezaji wa kibongo tunatofautiana vitu vidogo sana. Wengi tunakutana mitaani huku kwa hiyo hakuna tatizo ila kikubwa kufuata misingi iliyo bora," alisema beki huyo.

Miraji  alikuwa ni miongoni mwa mabeki bora wa kulia, lakini kukaa kwake nje ni kama kumemuondoa katika ramani lakini hilo yeye amelipinga.

"Naamini hilo linawezekana. Kuwa nilivyokuwa, linawezekana sababu najifunza kila siku na najifua pia kwa hiyo kikubwa uzima tu," alisema Miraji.

Miraji hapo nyuma aliwahi kuzichezea Simba, Coastal Union, Mtibwa Sugar, Singida United, Ndanda na pia amewahi kuzitumikia timu za taifa za vija ail echini ya umri wa miaka 17 na chini ya umri wa miaka 20.