Arsenal yarudi kivingine kwa Wilfried Zaha

Friday July 12 2019

 

WAKATI ARSENAL imerudi kivingine katika mbio zake za kumnasa winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha na sasa inataka kuipa Palace kiasi cha Pauni 40 milioni na wachezaji watatu kwa ajili ya kumnasa staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast.

Mastaa watatu ambao Arsenal inataka kuwatumia kama chambo katika mbio zake za kumnasa Zaha ni Calum Chambers, Mohamed Elneny na Carl Jenkinson ambao hawana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Kocha Unai Emery kuelekea msimu ujao.

Crystal Palace imemthaminisha Zaha kwa kiasi cha Pauni 80 milioni na dau hilo limekuwa gumu kwa Arsenal licha ya staa huyo kuiambia Palace kwamba anataka kujiunga na klabu hiyo aliyoishabikia tangu akiwa mtoto.

Manchester United iliweka kifungu cha kupewa asilimia 25 ya mauzo ya Zaha ilipomuuza kwa Palace ambayo ilishindwa kukiondoa katika dili la kumuuza Aaron Wan-Bissaka kwenda Old Trafford.

Advertisement