Liverpool yapanga mbinu ya kumpata Thiago Alcantara

Wednesday September 16 2020

 

LIVERPOOL inataka kusubiri hadi wiki ya mwisho ya dirisha hili la usajili ili kutoa tamko rasmi juu ya kiungo wa Bayern Munich, Thiago Alcantara ambaye imekuwa ikiisaka saini yake kwa muda mrefu.

Liver inataka kutumia mbinu hiyo ikiamini itamsainisha kwa bei ya chini tofauti na ikiamua kukamilisha usajili wake kwa sasa.

Manchester United ambayo ilikuwa kwenye vita hiyo, haionekani kuwa na shauku baada ya kuipata saini ya kiungo wa Ajax, Donny van de Beek hivyo Liver itakuwa yenyewe kwenye harakati hizo.

Thiago ambaye ana umri wa miaka 29, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2021 huku thamani yake katika soko la usajili ikiwa ni Euro 44 milioni.

Mhispania huyo alionyesha kiwango kikubwa akiwa na Bayern Munich kwa msimu uliopita na aliiwezesha kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu , Uefa na DFB-Pakal.

Advertisement