Recho avunja ukimya aja na wimbo Chocho

Thursday September 19 2019

Recho avunja, Mwanaspoti, ukimya aja, Tanzania, wimbo la Chocho

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam.Mwimbaji Recho amevunja ukimya kwa kufyatua wimbo mpya uitwao 'Chocho', akidai hii ni salamu kwa waiodhania amefulia.

Wimbo huo ambao umempagawisha mwanamuziki mkongwe Ray C ambaye mashabiki zao huwa wanawafananisha sauti na sura.

Ray C yuko nje ya nchi ameposti katika akaunti yake ya Instagram  kipande cha video ya wimbo wa ‘Chocho’  wa Recho na kuandika maneno haya :

‘Sauti ya kuzaliwa!!!Yani bila kufosi yani!!!!Yenyewe inajiachia Mashallah!SHE IS BACK!Nyoosha pacha nyoosha😘❤❤❤❤💪💪💪Ila mama sijui alichitigi kwa baba kha🤔😃😃’

Baada ya Posti hiyo baadhi ya watu katika comment wameomba Ray C na Recho wafanye wimbo wa pamoja. Moja ya Comment hizo ni:

“Daah yaani huyu kama wewe kabisa Ray C,pangeni siku moja mfanye kazi kwa pamoja itapendeza sana na hizo sauti zenu,” aliandika Selina Jacob

Advertisement

“Kwa kweli nyinyi ni ndugu kabisa, sio kwa kufanana huko na sauti hiyo, tunataka kazi moja au mbili mfanye kwa pamoja itahit sana.”

Aidha MCL Digital alizungumza na na Recho kuhusu ukimya wake alisema aliamua tu kuusoma mchezo, ila sasa amerejea kivingine kabisa.

Recho aliyewahi kutamba nyimbo kama Upepo, Kizunguzungu, Mwali Kigego, Nashukuru.

 

Advertisement