Mchawi wa Simba kwa Kagera Sugar huyu hapa

Wednesday September 18 2019

Michezo, Yanga, Mchawi wa Simba, Mwanaspoti, Tanzania, Kagera Sugar, huyu hapa

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa zamani wa Kagera Sugar, Edward Christopher aliyewaliza Simba msimu wa 2017/19 mbele ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema Simba inakuwa na hofu inapocheza na Kagera, ikiamini kuna mkono wa Yanga na kwamba hilo ndilo linalowaangusha.

Simba itacheza na Kagera Sugar, Septemba 26 ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa na timu hiyo misimu miwili mfululizo.

Akizungumzia unyonge huo wa Simba, Edo Christopher anayecheza anacheza Ruvu Shooting kwa sasa alisema Simba inakuwa na hofu inapocheza na Kagera, ikiamini kuna mkono wa Yanga.

"Nakumbuka wakati nipo Kagera Sugar ikifika wakati wa mechi ya Simba ama Yanga kocha alikuwa anatujenga na kutuaminisha kwamba wao ndio wanakuwa na presha ya kupata matokeo."

"Ili Simba iweze kuibuka na ushindi dhidi ya Kagera Sugar, basi wachukulie kama wanavyocheza na timu nyingine wanazozifunga, jambo lingine wanapokutana na timu za mikoani wanakuwa wanatamani kuonyesha ili na wao wapate nafasi ndani ya vikosi vyao," alisema Edo.

Advertisement