Yanga yatuma salamu kwa Township Rollers

Thursday August 8 2019

Yanga yatuma, salamu kwa, Tanzania, Township Rollers, Mwanaspoti, Mwanasport, Michezo, CAF, TFF

 

By Yohana Challe

Dar es Salaam.Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga jana usiku imeshinda ushindi wa kishindo wa mabao 4-1 dhidi ya Mlandege katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Yanga imepiga kambi visiwani humo kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers utakaopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

Mabao ya Yanga yaliwekwa kambani na Patrick Sibomana dakika ya 26, Mganda Juma Balinya dakika ya 36, Mnamibia Sadney Urikhob dakika ya 42 na Mrisho Ngassa dakika ya 65.

Bao pekee na la kufutia machozi la Mlandege SC lilifungwa na Hassan Ramadhani dakika ya 88.

Kocha Mwinyi Zahera ataendelea kunoa makali ya kikosi hicho kitakaposhuka uwanjani leo jikucheza na Malindi katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Tayari Yanga imecheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks, mwishoni mwa wiki iliyopita wakati timu hiyo ikiadhimisha Wiki ya Mwananchi' na kutoshana nguvu ya bao 1-1.

Advertisement

Advertisement