Hazard aaga kwa WhatsApp Chelsea

Wednesday June 19 2019

 

London, England. Eden Hazard ametambulishwa rasmi katika klabu yake mpya ya Real Madrid, lakini hakusita kuwakumbuka nyota aliocheza nao Chelsea.

Muda mfupi kabla ya kutambulishwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, Hazard alituma ujumbe mfupi wa maneno kupitia ‘WhatsApp’ akiwaaga nyota wa Chelsea.

“Asente, nawapenda,” aliandika nahodha huyo wa Ubelgiji kabla ya kujiondoa katika kundi la wachezaji wa Chelsea.

Mchezaji wa Chelsea, Emerson Palmieri alisema baada ya mchezaji huyo kuandika ujumbe huo, ameamini hatakuwa naye msimu ujao.

Hazard alisubiri muda mrefu kujiunga na Real Madrid kabla ya mpango huo kukamilika mapema mwezi huu baada ya kutua Santiago Bernabeu kwa Pauni150,000 milioni katika usajili wa majira ya kiangazi.

“Alituaga kwa kutumbia kwaherini vijana, lakini wote hatukuwa tukifahamu jambo lolote,”alisema Emerson.

Advertisement

Hazard ana rekodi ya kucheza mechi 245 na kufunga mabao 85 katika kikosi cha Chelsea tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akitokea Lille ya Ufaransa.

Advertisement