Manula afichua mashuti ya mbali yanavyompita langoni Simba

Wednesday May 15 2019

 

By Olipa Assa

KIPA wa Simba, Aishi Manula amewataka mashabiki wake kuelewa inapotokea kafungwa mabao ya mbali, waelewe kwamba ni changamoto ya kazi na sivinginevyo.

Anasema hiyo ni taaluma yake hivyo anapenda afanye kazi kwa ubora ili aweze kufika mbali na kuwasisitiza kwamba hata timu pinzani zinakuwa na wachezaji bora.

"Najua nasemwa juu ya kufungwa mabao ya mbali na kuiona wapinzani wanakuwa kwenye kiwango cha juu na mpira una ushindani ambao unakuwa na matokeo ya aina tatu kufungwa, sare na suluhu.

"Simba na Yanga asili yao hawapendi kufungwa na hawajawahi kukubaliana na aina tatu za matokeo mabao ninayofunga mimi angefunga Jonas Mkude ama Ibrahim Ajib basi inakuwa ndio habari ya mjini kuzifunga timu za mikoani.

"Lakini pia wanasahau hao wachezaji ambao wanafanya vizuri wanawatoa kwenye timu za mikoani, mfano mtu kama Shiza Kichuya wasingemsajili Simba kutoka Mtibwa Sugar kama angekuwa hana uwezo.

"Pamoja na hilo nafasi yangu ya kipa ngumu kuonekana nafanya mazuri, yanaonekana mabaya ili niweze kufika mbali zaidi napaswa kuangalia mbele na sio nyuma"anasema.

Advertisement

Advertisement