Katibu Singida United akiri ukata umewamaliza

Wednesday March 25 2020

 Katibu Singida United akiri ukata umewamaliza,Katibu Mkuu wa Singida United, Festo Sanga ,

 

By Mustafa Mtupa

Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Singida United, Festo Sanga amekiri ukata umefanya timu yao kufikia katika hatua mbaya ya sasa.

Sanga alisema hali mbaya ya kiuchumi ndiyo iliwafanya wao wasajili wachezaji wasiokuwa na ubora mkubwa kama ilivyokuwa misimu iliyopita.

“Shida ni kwamba tulikosea kwenye kufanya usajili, tulikuwa na lundo kubwa la wachezaji vijana ambao hawakuwa na uzoefu na Ligi Kuu hivyo ndo amana tukashindwa, pia mpira wa miguu unahitaji pesa na sisi kwa sasa tupo vibaya kiuchumi.”

Singida United inaburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi Ku, ikiwa imeshacheza michezo 29 na kukusanya point 15 tu.

Advertisement