Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Xavi aanza na suhindi Barca

Xavi aanza na suhindi Barca

KOCHA mpya wa Barcelona, Xavi ameanza na neema kwenye kibarua chake cha kuinoa miamba hiyo ya soka la Hispania baada ya kuiongoza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Espanyol kwenye mchezo wa Ligi Kuu Hispania 'La Liga'.

Katika mchezo huo wa dabi, ilimbidi Xavi kusubiri hadi kipindi cha pili ambapo Memphis Depay aliifungia bao Barcelona kwa mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa akiwa kwenye eneo la hatari.

Ushindi huo umeifanya Barcelona kusogea hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa La Liga huku wakiwa na pointi 20 walizozikufanya kwenye michezo 13, wameachwa kwa pointi nane na vinara wa ligi hiyo, Sevilla.

Xavi, ambaye aliichezea Barcelona michezo 767 na kutwa mataji  25 ndani ya miaka 17, ilimbidi kusubiri kwa wiki mbili kufuatia uwepo wa michezo ya kimataifa kabla ya kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo wake wa kwanza tangu arithi mikoba ya Ronald Koeman.

Mchezo ujao kwa Xavi akiwa na Barcelona utakuwa Jumanne kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo wataikaribisha  Benfica kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp.